Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya Kiswahili inatusaidia sana kwenye ulinzi wa amani DRC- Luteni Kanali Mley 

Lugha ya Kiswahili inatusaidia sana kwenye ulinzi wa amani DRC- Luteni Kanali Mley 

Pakua

Lugha ya Kiswahili hivi sasa ni lugha ya kimataifa ikiwa imetengewa siku yake mahsusi ya kuadhimishwa ambayo ni tarehe 7 Julai kila mwaka. Wakati wa maadhimisho ya mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, Audrey Azoulay alisema uamuzi wa Baraza Kuu la UNESCO kutambua lugha ya kiswahili kimataifa ulizingatia mambo kadhaa ya msingi ikiwemo nafasi ya lugha hiyo katika kusongesha amani. Na hilo linafanyika tayari huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kama anavyoelezea Kamanda wa Kikundi cha tisa cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-9 kinachohudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO. Kamanda anaanza kwa kujitambulisha katika makala hii iliyofanikishwa na Denisia Lihaya wa TANZBATT-9 na kusimuliwa na Assumpta Massoi. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Assumpta Massoi
Sauti
3'49"
Photo Credit
TANZBATT 9