Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya Kiswahili imenipa ajira Umoja wa Mataifa

Lugha ya Kiswahili imenipa ajira Umoja wa Mataifa

Pakua

Kutana na Priscilla Lecomte, mtaalamu wa mawasiliano wa UN-CBi, mpango unaoratibiwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP kushirikisha sekta binafsi katika kujiandaa kukabliana na majanga na hata kurejea katika hali nzuri baada ya majanga. Bi. Lacomte ni mzaliwa na raia wa Ufaransa ambaye anaamini lugha zina mchango mkubwa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu akitolea mfano lugha aanayoipenda, Kiswahili ambayo alianza kujifunza akiwa kwao Ufaransa kabla ya kubobea aliposafri na kuishi Afrika Mashariki na baadaye kupata kazi katika Umoja wa Mataifa ambako alitumia na anaendelea kutumia Kiswahili katika kazi zake.

Audio Credit
Anold Kayanda/Priscilla Lecomte
Audio Duration
2'31"
Photo Credit
UN/Assumpta Massoi