Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 JULAI 2022

14 JULAI 2022

Pakua

Jarida la leo lina Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Jifunze Kiswahili.

Katika Habari kwa Ufupi, Leah Mushi anamulika wito wa UNHCR wa kutaka sitisho la mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako watu wanauawa na maelfu wanafurushwa. Kisha anamulika ripoti ya Umoja wa Mataifa kuwa ujira wa wanawake kwenye sekta ya afya ni wa chini kulinganisha na wanaume hata kama wako katika ngazi moja na mwisho ni wito kutoka UNCTAD wa kutaka bara la Afrika lisitegemee tu mazao na madini kupata fedha za kigeni bali iuze bidhaa za kihuduma.

Mada kwa Kina inapiga kambi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia wadau wa Kiswahili wakipigia chapuo matumizi ya lugha hiyo katika kufundishia nchini humo.

Na kwenye kujifunza Kiswahili tunakwenda Uganda kwa Aida Mutenyo ,Mkuu wa Idara za Kiswahili za Vyuo Vikuu Afrika Mashariki akichambua methali “liandikwali ndilo liwalo.”

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'15"