Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 JULAI 2022

11 JULAI 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunamulika masuala ya idadi ya watu na amani Sudan Kusini. Katika idadi ya watu ikiwa leo ni siku ya idadi ya watu duniani tunajulishwa kuwa ifikapo tarehe 15 mwezi Novemba mwaka huu idadi ya watu duniani itafikia bilioni 8! Na miongoni mwa nchi ambazo idadi ya watu inaongezeka ni Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katika masuala ya amani huko Sudan Kusini mafunzo yameendeshwa ili jamii iweze kuwa sehemu ya kukabiliana na ukatili ikiwemo wa kingono. Makala  inakupeleka Mexico kwa msichana  ambaye ndoto yake ya kuwa mkunga ili kusaidia jamii yake imetimia. Mashinani ni nini kifanyike kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu? Karibu sana na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'58"