Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

07 JULAI 2022

07 JULAI 2022

Pakua

Hayawi hayawi sasa yamekuwa na leo jarida linajikita katika maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani kuanzia habari kwa ufupi ambayo imebisha hodi Paris Ufaransa kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, halikadhalika Zanzibar ambako huko Jumuiya ya Afrika MAshariki imekuwa na maadhimisho maalum bila kusahau kauli ya Gertrude Mongela kuhusu hatua ya Kiswahili kutambulika kimataifa. Mada kwa kina Flora Nducha amepiga kambi kwenye  ukumbi hapa Makao Makuu ya UN kwenye maadhimisho yaliyoongozwa na Tanzania, UNESCO, Jumuiya ya SADC na wadau wengine wengi. MAshinani ni kwa mwandishi wa vitabu wa kwanza mwanamke nchini Kenya kwa lugha ya Kiswahili. Karibu na mwenyeji wako ni Leah Mushi.

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
10'44"