Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuilinde bahari ili itulinde- Guterres

Tuilinde bahari ili itulinde- Guterres

Pakua

Mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Lisbon Ureno ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni lazima kubadili mwelekeo na mwenendo wa shughuli za binadamu kwa bahari la sivyo uchafuzi wa bahari utavuruga  harakati zote za kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Ndivyo alivyokuwa anatamatisha hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo huko Lisbon kwa lugha ya kiswahili kwenye mkutano huo wa baharí ulioandaliwa kwa pamoja na Kenya na Ureno.

Guterres amesema Bahari inatupeleka popote  kwa kuzingatia kuwa inaweza kufungua fursa mpya na mustakabali endelevu iwapo itatunzwa na kuwa na afya kwa sababu, “ni tegemeo la lishe kwa zaidi ya watu bilioni moja. Ni chanzo cha ajira kwa watu wapatao milioni 40. Na baharí yenye afya na fanisi ni muhimu kwa mustakabali wetu wa pamoja.”

Hata hivyo amesema hali ni tete, “hatukujali baharí hadi tunakabiliwa na kile ninachokiita dharura ya baharí.”

Amesema kiwango cha maji ya bahari kinaongezeka, visiwa vidogo vinazama, kiwango cha tindikali kwenye baharí kinaongezeka na takribani asilimia 80 ya majitaka yanaingia baharini bila kuondolewa sumu.

Ametaja mambo manne ya kuzingatiwa kuwa ni pamoja na,  Mosi, wadau wote kuwekeza kwenye matumizi endelevu ya baharí. Pili Bahari iwe muundo wa kuonesha jinsi ya kutumia kwa pamoja rasilimali kwa faida ya wote, tatu; sote lazima tulinde baharí na watu wanaoishi na kuitegemea na nne, sayansi na ugunduzi vituchagize kufungua sura mpya ya hatua za kulinda baharí.

 Kwa upande wake, Rais Uhuru Kenya wa Kenya akihutubia mkutano huo amesisitiza umuhimu wa vijana kuwa kiti cha mbele kwenye majadiliano akisema, “hatua za kuhamasisha dhidi ya baharí walizowasilisha jana, imeonesha kuwa vijana ni sehemu ya majawabu.”
 

Audio Credit
Anold Kayanda/Assumpta Massoi
Audio Duration
2'3"
Photo Credit
Ocean Image Bank/Vincent Knee