Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakazi wa Embu kwa msaada wa IFAD na serikali Kenya wamepanda miti na kulinda mazingira

Wakazi wa Embu kwa msaada wa IFAD na serikali Kenya wamepanda miti na kulinda mazingira

Pakua

Kenya ni moja ya nchi zilizoathirika sana na ukame uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi katika Pembe ya Afrika, lakini sasa baadhi ya wakulima wa nchi hiyo kwa msaada wa mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD wameamua kuchukua hatua kulinda mazingira, maisha yao na kujenga mnepo kwa kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Katika kaunti ya Embu wakulima wamepanda msitu mpya ambao unawapa sio tu jukumu jipya la kuulinda lakini pia kuwa chanzo cha kuwapatia kipato.

Audio Credit
Leah Mushi/ Flora Nducha
Audio Duration
2'58"
Photo Credit
IFAD/ Video Capture