Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgeni njoo mwenyeji apone ndio hali wakulima Lodwar baada ya ujio wa WFP na FAO

Mgeni njoo mwenyeji apone ndio hali wakulima Lodwar baada ya ujio wa WFP na FAO

Pakua

Kutana na Agnes mkulima kutoka wilaya ya Lodwar kaunti ya Turkana jimbo la Rift Valley nchini Kenya. Mabadiliko ya tabianchi yanayolikumba eneo la Afrika Mashariki kwa kiasi kikubwa yamemuathiri sana yeye na jamii yake, lakini sasa asante kwa mradi wa pamoja wa mashirika ya Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na la chakula na kilimo FAO wa kuwasaidia wakulima wadogo kujenga mfereji wa maji kwa ajili ya umwagiliaji na kununua mazao yao, maisha ya Agnes na jamii yake yamebadilika.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Flora Nducha
Audio Duration
2'36"
Photo Credit
©FAO/Kenya Team