Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

17 MACHI 2022

17 MACHI 2022

Pakua

Miongoni mwa yaliyomo leo katika jarida letu la Habari linaloletwa kwako na Leah Mushi

- Mswada mpya unaopendekewa Uingereza kuhusu uhamiaji hauna tija kwa wakimbizi, waomba hifadhi na wahamiaji yaonya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na kutoa raia kwa serikali ya nchi hiyo kuufikiria upya

-Huko Gambia mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa la ufadhili kwa kilimo IFAD waleta nuru kwa wakulima wa mpunga ambao pia wanafanya biashara

-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kikosi cha 8 cha Tanzania TANZBATT 8 kilichomaliza muda wake chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kinajivunia mafanikio makubwa yenye tija kwa wananchi.

-Makala yetu leo inatupeleka Uganda wilayani Hoima kuangazia changamoto na athari za mafuriko kwa wanawake wa kikundi cha Kaiso Women Group (KWG)

-Na mashinani tunabisha hodi Lviv Ukraine kwake Nataliya Ambarova mfanyakazi wa kujitolea anasimulia jinsi machungu wanayopitia wakimbizi wa ndani nchini Ukraine 

Audio Credit
Un News/ Leah Mushi
Audio Duration
13'49"