Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko yavuruga ndoto za wanawake wa Ziwa Albert, Uganda

Mafuriko yavuruga ndoto za wanawake wa Ziwa Albert, Uganda

Pakua

Mbali na janga la Janga la Corona au COVID-19 ambalo limeikumba dunia kwa zaidi ya miaka miwili, wananchi wa Uganda waishio karibu na Ziwa Albert kwa miaka hiyo miwili wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ziada ya mafuriko.

Wanawake wanachama wa kikundi cha Kaizo Women’s Group (KWG) wilayani Hoima ni moja wapo ya vikundi ambayo mipango yao ilikwamishwa na atahri za mafuriko na ambao sasa wanaomba msaada wa kifedha kutoka serikali katika juhudi zao za kujikwamua kutokana na uharibifu wa maji huku wakikabiliana na janga la COVID-19.

Mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego amefanya mahojiano na Ongyera Aness afisa wa ujasiriamali katika kikundi hicho.

 

Audio Credit
UN News/ John Kibego- stringer
Audio Duration
3'32"
Photo Credit
© UNICEF/Zahara Abdul