Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila vikwazo kuanzia ngazi ya familia, wanawake wana mchango mkubwa na chanya kwa jamii

Bila vikwazo kuanzia ngazi ya familia, wanawake wana mchango mkubwa na chanya kwa jamii

Pakua

Miradi mbalimbali inayotekelezwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake kote duniani, imeweka wazi ukweli kwamba vikwazo mbalimbali vinavyowakabili wanawake vinapoondolewa, wanawake wanakuwa chachu ya kuleta mabadiliko chanya katika karibia kila sekta katika jamii. Mfano wa karibu ni katika mkoa wa Kigoma nchini Tanzania ambako kupitia mradi wa pamoja Kigoma, KJP chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, Shirika la Umoja wa mataifa la maendeleo ya mitaji UNCDF na Kituo cha Biashara cha kimataifa ITC, wanawake sasa wanatoa mchango mkubwa wa maendeleo katika jamii yao. John Kabambala wa redio washirika wetu KidsTime ya Morogoro Tanzania alifika mkoani Kigoma kuyashuhudia hayo na kuandaa makala.

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kabambala
Audio Duration
4'
Photo Credit
FAO Tanzania