Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikundi vya kilimo Kigoma vyaondoa utegemezi wa wanawake

Vikundi vya kilimo Kigoma vyaondoa utegemezi wa wanawake

Pakua

Nchini Tanzania hususan mkoani Kigoma, mafunzo ya kilimo hifadhi yanayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo yamejengea uwezo wanawake na sasa wana uwezo sio tu wa kukidhi mahitaji yao bali pia kulipa gharama za pembejeo za kilimo. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.

Kazi ya kupura maharagwe yaliyovunwa kutoka shambani ikiendelea hapa kwenye makazi ya mkulima Grace Jackson Ntaziha, mkazi wa kata ya Kitahana, kijiij cha Kitahana wilayani Kibondo mkoani Kigoma nchini Tanzania.

Bi.Ntaziha ni miongoni mwa wakulima walionufaika na mafunzo ya kilimo hifadhi ambacho pia kinatumia mbegu ya kisasa.

Mkulima huyu ambaye sasa anaona faida ya kilimo anasema ameondokana na adha ya kukosa fedha na akatoa wito kwa wanawake wenzake hasa wakati huu wa kuelekea siku ya wanawake duniani tarehe 8 mwezi huu wa Machi ikiwa na maudhui ya Usawa wa kijinsia kwa mustakabali endelevu.

Mafunzo haya ya kilimo hifadhi yanatolewa na FAO chini ya mradi wa pamoja wa Kigoma, KJP unaotekelezwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo FAO.

Programu ya pamoja kwa mkoa wa Kigoma ilianza mwaka 2017 na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika ni pamoja na lile chakula na kilimo, FAO, mpango wa chakula, WFP, kituo cha biashara cha kimataifa, ITC na lile la maendeleo ya mitaji, UNCDF.

Audio Credit
Leah Mushi/Assumpta Massoi
Audio Duration
2'37"
Photo Credit
© WFP/Fredrik Lerneryd