Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Save the children waendelea na misaada ya kibinadamu Madagascar

Save the children waendelea na misaada ya kibinadamu Madagascar

Pakua

Nchini Madagascar, mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa bado yanahaha kuwasaidia wananchi wa taifa hilo ambao kwa mfululizo katika kipindi cha muda mfupi mwezi uliopita wamepigwa na vimbunga vinne yaani Ana, Batsirai, Emnati na Dumako ambavyo vimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na ustawi wa watu. Ripoti iliyotolewa na serikali ya Madagascar inaonesha kwamba watu 400 000 wameathirika na vimbunga Emnati na Batsirai.

Takriban hekta 60, 000 za mashamba ya mpunga zimefurika maji, na kuleta hofu kuhusu mavuno yajayo, hasa katika baadhi ya maeneo yanayokumbwa na hali ya njaa. Hadi leo watoto 200,000 hawapo shuleni, madarasa yao yakiwa ama yamebomoleka au yametumiwa kama makazi ya muda. 

Moja ya mashirika yaliyoingia nchini Madagascra kuongeza nguvu ya msaada ni Save the Children. Ili kufahamu shirika hilo la Save the Children linatoa msaada gani, Priscilla Lecomte ni afisa mawasiliano katika timu ya dharura ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA amezungumza na Jeremiah Kariuki afisa wa shirika hilo la la kimataifa linalolenga kuboresha maisha ya watoto duniani. 

 

Audio Credit
Leah Mushi /Priscilla Lecomte
Audio Duration
3'33"
Photo Credit
Viviane Rakotoarivony for OCHA