Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani aanza ziara DRC
Pakua
Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix leo ameanza ziara ya siku tatu nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC, kumuwakilisha Katibu Mkuu. Ziara hiyo imeanzia Bunia Mashariki mwa DRC ambako amezuru kambi ya wakimbizi wa ndani, kuzungumza nao na kushudia hali halisi lakini pia kuzungumza na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.
Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ni miongoni mwa walioambatana na Lacroix ametuandalia taarifa hii.
Audio Credit
Leah Mushi/Assumpta Massoi
Audio Duration
1'41"