Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FISH4ACP wahifadhi mazingira ya Ziwa Tanganyika nchini Tanzania

FISH4ACP wahifadhi mazingira ya Ziwa Tanganyika nchini Tanzania

Pakua

Mkoani Kigoma nchini Tanzania wavuvi katika ziwa Tanganyika waliopatiwa mafunzo na FAO Tanzania kupitia mradi wake wa Fish4ACP sasa wana mtazamo tofauti na ule waliokuwa nao kabla ya kupatiwa mafunzo kwa kuzingatia kuwa ukosefuwa elimu ya uhifadhi wa mazingira huleta madhara katika nyanja mbalimbali, madhalani baadhi ya wavuvi wanaotumia mbinu za asili bila kujali mazingira wanaweza kusababisha kupungua kwa viumbe maji na hata kukosekana kwa mazao ya uvuvi.  Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM anafafanua zaidi.

Sasa wavuvi wanachukua hatua akiwemo Charles Rubaka ambaye ni mvuvi katika Mwalo wa Kibirizi anasema uvuvi wa asili huchangia kuharibu mazingira yanayozunguka Ziwa Tanganyika.

Mbali na hayo Charles akaiomba serikali kuweka mikakati thabiti ya uhifadhi wa mazingira wakati wote. 

Safi Mwisigalo mfanya biashara katika Mwalo wa Kibirizi anaeleza wanavyoshiriki katika utunzani wa mazingira.

Afisa Uvuvi Halmashauri ya Kigoma UJiji, Malick Kibetele anaeleza namna serikali inaboresha miundombinu ya uvuvi.

Benjamin Dotto ambaye ni Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi  na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) anatuhitimishia Makala haya kwa kueleza mikakati yao.

Audio Credit
Leah Mushi/Devotha Songorwa
Audio Duration
3'17"
Photo Credit
UN Tanzania