Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR ina wasiwasi na namna watu wa Asili nchini Venezuela wanavyoishi

UNHCR ina wasiwasi na namna watu wa Asili nchini Venezuela wanavyoishi

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa wasiwasi mkubwa na mazingira dunia wanaoishi wakimbizi na wahamiaji kutoka jamii ya Warao nchini Venezuela ambao kwa sasa wanaishi Guyana. Watu hao wanaishi katika maeneo ambayo ni vigumu kufikika na wanakosa huduma za msingi zikiwemo za afya, malazi, chakula na elimu.

Sasa UNHCR na wadau wamelivalia njuga suala lao kwa kuwafikishia misaada. Jason Nyakundi na taarifa kamili. 
Natss…..Nello 
Huyo ni Nello kiongozi wa jamii ya watu wa asili ya Warao kutoka Venezuela ambao kwa sasa wanaishi katika ufukara mkubwa kama kama wakimbizi na wahamiaji kwenye maeneo ya vijijini karibu na mpaka baina ya Venezuela na Guyana.  

Anasema walilazimika kusafiri kuja kusaka hifadhi kwa kitumia ngalawa usiku kucha na mchana kutwa kwa siku mbili ili kuweza kufika hapa kijijini Kaituma Guyana. 

Nello ni mmoja kati ya Warao 2,500 wanaopata hifadhi hapa wakiwani sehemu ya wakimbizi  na wahamiaji 24,000 kutoka Venezuela waliongia Guayana na zaidi ya nusu yao ni watoto , na Nello alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasili katika eneo hilo 

“Tulikuja kwa kutumia ngalawa kubwa tatu na eneo lote hili lilikuwa pori. Tulikuwa wa kwanza kufika, mimi, baba mkwe wangu, binamu zangu na familia yangu, na kisha familia zingine zikawasili na zingine bado zinaendelea kuja kutoka jamii zingine.” 

Pamoja na kwamba wamepata hifadhi  na wako salama lakini UNHCR inawasiwasi kwani inasema fursa ya kupata huduma za msingi ni finyu hasa kutokana na kwamba wako ndanindani vijijini, hali mbaya ya uchumi, miundombinu duni na na janga la COVID-19

Tathimini ya karibuni ya UNHCR imeonyesha kwamba wakimbizi wengi wa jamii ya Warao wanalazimika kula mlo mmoja tu kwa siku, kwani hawawezi kumudu zaidi ya mlo mmoja na hakuna fursa za ajira, familia nyingi hazina maji safi na salama ya kunywa zinategemea maji ya mto kwa kila kitu na vifaa vya kujikinga na COVID-19 kama barakoa ni mtihani kupata. 

UNHCR kwa kushirikiana na wadau wengine wa kibinadamu sasa imeanza kuwasambazia msaada muhimu ikiwemo chakula, taa za kandili inazotumia sola, barakoa, vyandarua vya mbu, tembe za kusafisha maji na misaada mingine ya muhimu na tayari watu 400 wa jamii ya Warao wameshapokea msaada.

Lengo la UNHCR ni kuendelea kusambaza msaada zaidi ili kuwafikia wakimbizi wote 24,000 walioko Guayana. 

Audio Credit
Flora Nducha / Jason Nyakundi
Audio Duration
2'43"
Photo Credit
© UNHCR/Diana Diaz