Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto DRC wataka washirikishwe kwenye mazungumzo ya mabadiliko ya tabianchi

Watoto DRC wataka washirikishwe kwenye mazungumzo ya mabadiliko ya tabianchi

Pakua

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linatumia mabalozi wake watoto ambao ni wachechemuzi kuhusu tabianchi kuelezea adha ambazo watoto wanapata kutokana na madhara ya tabianchi na nini wanataka kifanyike. 


Miongoni mwao ni Kestia mwenye umri wa miaka 17 ambaye anasema, 
“Nchi yangu DR Congo ni ya pili kwa kuwa na msitu mkubwa wa mvua duniani  na vyanzo vya maji ni asilimia 13 ya uwezo wa kuzalisha umeme kwa njia ya maji. Lakini bado watoto wa DR Congo wanasumbuliwa na mafuriko, mmomonyoko wa udongo na mvua kubwa na kwa sababu yah ii, hawawezi kwenda shule, hospitali na hawana huduma ya maji safi ya kunywa. Na kila wakati wao ndio wanaokumbwa na magonjwa hatari  kama vile kipindupindu na Malaria.” 

Kwa mujibu wa UNICEF, uchafuzi wa udongo unaohusiana na usimamizi mbovu wa uchimbaji madini ni tatizo kubwa kwa afya ya watoto na uharibu bayonuiai ya vizazi vijavyo.  

Ni kwa mantiki hiyo Kestia ana  ujumbe. “Tunataka hatua zichukuliwe ili kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Sisi watoto tunatoa wito kwa wadau wazingatie suluhu kwa tabianchi na walinde wale walio katika maeneo hatari zaidi. Hii leo natoa wito kwa ushiriki zadi wa vijana katika mazungumzo kuhusu masuala ya tabianchi katika ngazi ya kijamii, kitaifa na kimataifa. Vijana wana haki na pia ni wajibu wao kushiriki kwenye mustakabali wao.” 

Audio Credit
Flora Nducha/ Kestia
Audio Duration
1'32"
Photo Credit
Photo: UNFPA