Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi na wahamiaji hawaji kudoea bali wana mchango mkubwa pia:Profesa Gurnah

Wakimbizi na wahamiaji hawaji kudoea bali wana mchango mkubwa pia:Profesa Gurnah

Pakua

Mwishoni mwa wiki kamati ya kimataifa ya tuzo ya amani ya Nobel yenye makao yake makuu nchini Norway iliwatangaza washindi wa tuzo ya amani ambapo waandishi wawili wa Habari walishinda kutokana na mchango wao katika kusongesha na kupigania amani.

Tuzo hiyo ambayo ilianza kutolewa mwaka 1901 huwatunukia pia washindi wengine katika fani za Fizikia, Fiziolojia na madawa, Falsafa, Fasihi na uchumi. Na mwaka huu miongoni mwa washindi ni mwandishi wa vitabu mzaliwa wa Zanzibar Tanzania Profesa Abdilrazak Gurnah ambaye kwa sasa anaishi nchini Uingereza. Binafsi alikuwa mkimbizi alipoingia nchini humo katika miaka ya 1960 na ametunukiwa tuzo katika fani ya Fasihi kutokana na  mchango wa uandishi wake wenye huruma katika masuala ya ukoloni na hatma ya wakimbizi na wahamiaji.

Amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuhusu tuzo aliyopata. 

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'55"
Photo Credit
Dennis DeCaires