Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Tanzania ahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76

Rais wa Tanzania ahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76

Pakua

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani ikiwa ni mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo mwezi Machi mwaka huu, huku akimulika masuala mbalimbali kuanzia uchumi, siasa, tabianchi, COVID-19 na usawa wa jinsia. 

Rais Samia alikaribishwa ukumbini na Mwenyekiti Mwenza wa kikao cha leo cha mkutano wa UNGA76.

Taarifa zaidi na Flora Nducha

Katika hotuba yake ya kwanza ana ka kwa ana kwenye mjadala huo amezungumzia masuala mbalimbali yaliyo na umuhimu wa kitaifa na kimataifa akianza na suala la ushirikiano wa kimataifa.

Akizungumzia ushirikiano wa kimataifa amesema “Chini ya uongozi  wangu Tanzania itaendelea kuwa mshika muhimu wa Umoja wa Mataifa na muungaji mono wa kutegemewa wa suala la ushirikiano wa kimataifa tutanyoosha mkono kwa wale wanautukumbatioa na kushirikiana nasi. Tutaendelea kuwa Tanzania mambayo mmeifahamu kwa muda mremu, Tanzania yenye amani na ambayo inashirikiana nan chi zote, kubwa au ndogo, zenye nguvu au zisizo na nguvu, Tajiri au masikini kuifanya dunia dunia yetu kuwa bora kwa ajili yetu sote.”

Na katika upande  COVID-19 Rais Samia akafunguka akisema, “Janga COVID-19 limetukumbusha jinsi gani tulivyo hatarini kama nchi bila kujali ukubwa , utajiri au wapi tulipo. Tunapokutana hapa leo tumebakiza chini ya muongo mmoja ili kutimiza lengo letu la pamoja kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kwa masikitiko makubwa nimebaini katika ripoti ya malengo ya maendeleo endelevu ya 2020 kwamba dunia imeenda kombo katika kutimiza malengo haya kutokana na athari za COVID-19.”

Rais Samia Hassan mbali ya kuhutubia mjadala wa Baraza kuu pia anashiriki mikutano mingine mbalimbali ya ngazi ya inayojikita na mbada mbalimbali miongoni mwao ni mabadiliko ya tabianchi, mifumo ya chakula, masuala ya nishati, malengo ya maendeleo endelevu na COVID-19.

Kwa kina kuhusu yote aliyoyazungumza kwenye mjadala huo fuatilia wavuti wetu www. news.un.org/sw  na kwenye twitter na YouTube @ Habari za UN.

Mwaka huu wakuu wa nchi na serikali zaidi ya 100 wameshiriki mjadala huu wa UNGA76 ana kwa ana kwenye makao Makuu mjini New York huku wengine wakishiriki kwa njia ya mtandao.

Audio Credit
Assumpta Massoi / Flora Nducha
Audio Duration
1'52"
Photo Credit
UN/Cia Pak