Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wa UMoja wa Mataifa waimarishiwa teknolojia ya kidigitali

Walinda amani wa UMoja wa Mataifa waimarishiwa teknolojia ya kidigitali

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres hii leo katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani amezindua ‘Mkakati wa Mabadiliko ya Kidigitali ya Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa’. 

(Taarifa ya Flora Nducha/Anold Kayanda) 
Mkakati huu wa mabadiliko ya kidijitali ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa unaolenga kuwawezesha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kote duniani kuendana sawa na maendeleo ya kidijitali, umezinduliwa na Katibu Mkuu Guterres wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likikutana katika mjadala wa wazi kuhusu ulinzi wa amani  na teknolojia na azimio la kuwalinda walinzi.  

Aidha inaelezwa kuwa mkakati unakusudia kuwezesha ujumbe kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi na kuimarisha usalama na walinda amani kwa kutumia uwezo wa teknolojia za dijiti na pia kupunguza hatari, huku ukiweka ulinzi wa amani kuendelea kubadilika katika matumizi yake ya teknolojia. 

Mikakati ya Katibu Mkuu kuhusu Teknolojia Mpya na Takwimu inaweka fursa kwa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kutengeneza njia yake kutumia uwezo wa teknolojia katika kusimamia vizuri huduma na mamlaka yake sasa n ahata kwa siku zijazo.

Katika mpango wake wa Ushirikiano wa kidijititali, Katibu Mkuu Guterres anatambua kuwa, "teknolojia za dijitali zinaweza kusaidia juhudi za kulinda amani za Umoja wa Mataifa ulimwenguni, pamoja na kuhakikisha usalama na usalama wa walinda amani." 

Maono ya uwezo zaidi wa ndani wa matumizi ya teknolojia mpya yanaendana na mpango wa Hatua ya Ulinzi wa Amani, A4P; vipaumbele vya A4P Plus, A4P + vya 2021 ambavyo vinasisitiza ulinzi wa amani unaotokana na ubinifu, takwimu na  teknolojia. 

Wavuti rasmi wa Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa, “teknolojia za dijitali zinachukua jukumu muhimu na gumu zaidi katika eneo la migogoro. Wanaunda mazingira ya mizozo na wanaathiri tabia na matendo ya watendaji wa mizozo. Teknolojia za kidijitali husababisha hatari mpya lakini pia zinaonesha fursa mpya za kuboresha ufanisi wa shughuli za kulinda amani na usalama na usalama wa walinda amani.”
 

Audio Credit
Flora Nducha /Anold Kayanda
Audio Duration
1'58"
Photo Credit
UN Photo/Sylvain Liechti