Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kabla ya kupokea mgao, tulikula mlo mmoja tu, lakini tangu tupate fedha za msaada tunakula milo miwili kwa siku : Mnufaika Zambia

Kabla ya kupokea mgao, tulikula mlo mmoja tu, lakini tangu tupate fedha za msaada tunakula milo miwili kwa siku : Mnufaika Zambia

Pakua

Nchini Zambia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake wameleta nuru kwa kaya maskini ambazo zimeshuhudia maisha  yao yakienda mrama baada ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 kubisha hodi kwenye taifa lao mwezi Machi mwaka jana. Sasa kaya hizo zinapatiwa fedha taslimu za kujikimu kila mwezi na kando ya kutumia zimeamua kuwekeza kwenye biashara.

Taarifa ya Jason Nyakundi

Kutana na William Simazuba, baba huyu wa familia nchini Zambia na mmoja wa wanufaika wa mradi wa serikali ya Zambia unaoungwa mkono na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia watoto UNICEF, la kazi, ILO na wadau kama vile serikali ya Ujerumani.
Simazuba anasema “tangu kuanza kwa janga la Corona, ilikuwa ni vigumu sana kupata mlo kwa ajili ya familia yangu.”
Serikali ya Zambia na wadau wake mwezi Julai mwaka 2020 walizindua mradi wa mgao wa fedha za dharura au ECT kwa kaya maskini, ambapo jumla ya kaya Laki Mbili  katika wilaya 22 zilipatiwa kila kaya dola 18 kila mwezi kwa kipindi cha miezi sita.  

Fedha zililipwa kwa miezi miwili miwili au mitatu mitatu katika 
Simazuba akiwa kwenye kibanda chake cha biashara anasema, “fedha nilizopokea, niliwekeza katika biashara yangu  Kwacha 1,500  sawa na dola 66. Fedha zilizobakia nililipa ada za shule za watoto wangu na pia nimenunua chakula. Sababu ya kuwekeza ni kwamba ziweze kuongezeka ili ninunue chakula cha kutosha cha familia.”
Akiwa mbele ya nyumba yake Simazuba anakumbuka kuwa kabla ya kupokea mgao, walikula mlo mmoja tu kwa siku, lakini tangu apate fedha hizo wanakula milo miwili kwa siku.
Anatamatisha akisema “mgao huo wa fedha umenisaidia sana, nashukuru mno,”

Mnufaika mwingine ni Joyce Mutaipe. Bibi huyu akiwa mbele ya genge lake anasema, “mgao niliopokea nilinunulia cherehani na kumpatia mjukuu wangu  atumie ili tupate fedha za kununulia chakula baadaye. Fedha nyingine nimenunua chakula Tunashukuru sana kwa msaada.”

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Jason Nyakundi
Audio Duration
2'8"
Photo Credit
© UNICEF/UN0391492/Siakachoma/OutSet Media