Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Peninah Wanja, msomi wa ufugaji ahudumia wafugaji Kenya kidijitali

Peninah Wanja, msomi wa ufugaji ahudumia wafugaji Kenya kidijitali

Pakua

Uvumbuzi ni moja ya malengo 17 ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs. Vumbuzi mbalimbali zinazotokea duniani hasa kutokana na ukuaji wa teknolojia, kwa asilimia kubwa zinachangia katika kubadilisha maisha ya watu kuwa mazuri kiuchumi, kiafya au katika maisha yao kila siku na hivyo kukuza ustawi wa wakazi wa ulimwengu. Nchini Kenya uvumbuzi uliofanywa na Peninah Wanja wa Apu ya simu kwa jina DigiCow umewasadia wakulima wafugaji wa ng’ombe kupata huduma muhimu kwa njia rahisi na ya haraka kwa kuwaunganisha wakulima na wataalamu wa afya ya mifugo. Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na Peninah kuhusu uvumbuzi huo.
 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'42"
Photo Credit
FAO/Franco Mattioli