Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira kwa wakimbizi wazee ni adimu zaidi

Ajira kwa wakimbizi wazee ni adimu zaidi

Pakua

Ili kuweza kuishi maisha ya kistaarabu na staha niwajibu kuwa na shughuli ya kukuingizia kipato. Mzee Agapito Andrade mkimbizi raia wa Colombia anayeishi nchini Equador imekuwa ngumu kupata ajira na hivyo hata mlo kwake umekuwa tabu huku janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 likiongeza ugumu maradufu kupata ajira. Taarifa Zaidi tuungane na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Kila siku asubuhi, Agapito Andrade anaamka bila kufahamu  atakula milo mingapi kwa siku hiyo. Mkimbizi huyu raia wa Colombia mwenye umri wa miaka 65 hana ajira wala pensheni ambayo ingemuwezesha kuwa na fedha za kujikimu.

Kama maeneo mengine ya wakimbizi, imekuwa vigumu kwa Agapito kupata ajira rasmi katika nchi iliyompokea, kitu ambacho kimekuwa kigumu zaidi kutokana na janga la COVID-19.

 (Sauti ya Agapito) 

 "Siku nyingine, tunapata kwa tabu kifungua kinywa, hatuna chakula cha usiku na mara nyingine tunakosa kabisa kifungua kinywa, saa nyingine mimi na mke wangu tunapata mlo mmoja tu kwa siku"

Vilma Estacio, mke wa Agapito, mkunga raia wa Ecuador kutoka mji wa San Lorenzo unaopakana na Colombia anasema akipata fedha atanunua kuku akisema… 

 Anasema "Ninatoa huduma kwa wanawake wajawazito. Kama Watoto wamekaa vibaya tumboni, nawaweka vizuri. Nawachunguza hadi wakati wa kujifungua utakapofika. Nikilipwa nitatumia pesa hiyo kujinunulia kuku."

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Wakala wa wakimbizi wa umoja wa mataifa na Shirika la kuhudumia wazee – HelpAge, asilimia 64 ya watu wazima waliopo Amerika ya Kusini hawakuwa na uwezo wa kupata mshahara kila mwezi, na wale waliokuwa wakipata mshahara walieleza hauwatoshi kujikimu.

Neira Valencia katibu wa asasi ya wastaafu ya San Lorenzo anasema "hili janga limebadilisha kila kitu, huu umri wa watu wazima wazee kwa mfano kwenye mifuko ya hifadhi hawapati dawa zote wanazohitaji. Kwa mzee yeyote anayekuja hapa kutoka kokote kule kama ni Colombia au Venezuela milango iko wazi na tunawakaribisha."

Agapito bado anaendelea kusaka ajira ili aweze kujikimu. 

Audio Credit
Leah Mushi/Assumpta Massoi
Photo Credit
WFP/Jonathan Dumont