Skip to main content

Tusipolinda bayoanuai tunajiangamiza wenyewe:CBD

Tusipolinda bayoanuai tunajiangamiza wenyewe:CBD

Pakua

Tatizo la kutoweka kwa bayoanuai ambayo ni muhimili mkuu wa maisha ya dunia na viumbe vilivyomo linaongezeka kila uchao na mlaumiwa mkubwa ni binadamu na shughuli zake za kila siku. Mwishoni mwa wiki Dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya bayoanuai iliyobeba kaulimbiu  “sisi ni sehemu ya suluhu”  Umoja wa Mataifa umetoa rai kwa kila mtu kuwajibika kuilinda bayoanuai ambayo hakuna atakayesalimika bila hiyo . Takimu za Umoja wa Mataifa kupitia sekretariati yake ya mkataba wa kimataifa wa kulinda bayoanuai CBD, zimeonya kwamba bayoanuwai inapotea kwa kasi na janga la corona au COVID-19 limedhihirisha bayana umuhimu wa kuchukua hatua ili kuhakikisha binadamu wanaishi vyema na mazingira asilila kwa ajili ya mustakbali wa dunia na viumbe vilivyomo kwa sababu asilimia kubwa ya changamoto zimechangiwa na binadamu wenyewe.
Ili kufahamu zaidi Flora Nducha amezungumza na Elizabeth Mrema Katibu Mtendaji wa CBD, ambaye anaanza kwa kufafanua uhusiano wa bayoanuai na janga la COVID-19

Audio Credit
UN News/Flora Nducha and CBD Elizabeth Mrema
Audio Duration
9'5"
Photo Credit
UNDP/Ya'axche