Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

24 MEI 2021

24 MEI 2021

Pakua

-Katika jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Leah Mushi anakuletea 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo mjni Goma jimboni Kivu Kaskazini umesababisha vifo vya watu 15. 

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehutubia mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Shirika la afya la Umoja wa Mataifa Ulimwenguni, WHO na kusema iwapo ubaguzi katika utoaji chanjo dhidi ya COVID-19 utaendelea, nchi tajiri zitachanja watu wake  huku virusi vikiendelea kusambaa  katika nchi

-Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP limeimarisha msaada wa chakula katika maeneo yanayokabiliwa na njaa nchini Yemen kama sehemu ya kuzuia njaa lakini uwezo wa shirika hilo kuendelea na shughuli hadi mwishoni mwa mwaka ziko njia panda.  

-Mada kwa kina leo inajikita na suala la bayoanuai, jinsi COVID-19 ilivyoliathiri na nini kifanyike kuilinda

-Na Mashinani tunaelekea Ecuador kupata ujumbe kutoka kwa mwanaharakato kutoka jamii ya watu wa asili anayepigania haki za wanawake na kulinda bayoanuai.

Audio Credit
UN News/Leah Mushi
Audio Duration
11'10"