Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaonya kuwa hakuna dalili za kumalizika mzozo Tigray.

UNICEF yaonya kuwa hakuna dalili za kumalizika mzozo Tigray.

Pakua

Ripoti za kusikitisha zimeendelea kujitokeza za kusambaa kwa  unyanyasaji mkubwa wa raia katika eneo la Tigray nchini Ethiopia, karibu miezi sita tangu mzozo ulipozuka, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.  Flora Nducha na maelezo zaidi.

Katika taarifa ya shirika hilo iliyotolewa leo msemaji wa UNICEF James Elder aliyehitimisha zira jimboni humo hivi karibuni akizungumza na waandishi wa Habari mjini Geneva Uswis amesema "Hakuna dalili za dhahiri za kumalizika kwa mzozo katika jimbo hilo la Kaskazini mwa Ethiopia.” 

Wakimbizi wa ndani wakisubiri cheki kwa ajili ya kupata chakula Tigray, Ethiopia.
© UNICEF/Mulugeta Ayene
Wakimbizi wa ndani wakisubiri cheki kwa ajili ya kupata chakula Tigray, Ethiopia.

Hofu mbaya zaidi 

Ameongeza kuwa zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kuhama makazi yao, mapigano yanaendelea, na usalama unabaki kuwa suala lenye changamoto kubwa.  

Amesema “UNICEF ilikuwa na wasiwasi tangu mwanzo kuhusu  madhara ya mzozo huo kwa watoto, na kwa bahati mbaya hofu kama hiyo sasa inatekelezwa." 

Mzozo huo ni matokeo ya miezi kadhaa ya kuongezeka kwa mivutano kati ya Serikali kuu ya Ethiopia na jeshi kubwa la mkoa wa Tigray la People's Liberation Front (TPLF), mivutano ambayo ilimlazimu Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuagiza mashambulizi ya kijeshi baada ya waasi kushambulia kituo cha jeshi la serikali ya shirikisho. 

Ndani ya siku chache, wanamgambo kutoka eneo jirani la Amhara walikuwa wamejiunga na vita, ambayo inasemekana vilifuatiwa na askari wengine kutoka nchi jirani ya Eritrea ambayo ni mpinzani wa muda mrefu wa Tigray. 

Kwa mujibu wa Serikali, mkoa huo au jimbo hilo la Tigray lilikuwa limedhibitiwa mwishoni mwa Novemba mwaka jana, hata hivyo upinzani wa TPLF umeendelea, huku kukiwa na mashtaka ya mauaji ya kiholela na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kwa pande zote. 

Waathirika watoto 

Bwana. Elder amesisitiza kuwa athari za vita hivyo kwa wanawake na ni "mgogoro wa ulinzi". 

Ameongeza kuwa "Kinachojitokeza hivi sasa ni taswira ya kusikitisha ya ukiukaji mkubwa na unaoendelea dhidi ya watoto, na pia kwa bahati mbaya kuna dharura ya elimu na lishe na niliona ya uharibifu mkubwa kwa mifumo ya huduma muhimu ambazo watoto wanazitegemea." 

Miongoni mwa wanaokadiriwa  kuathirika na mzozo huo milioni moja ni watoto ambao wanateseka vibaya, ameeleza afisa huyo wa UNICEF.  

Mwendo wa kilomita 300 kusaka usalama 

Elder amesema "Nilizungumza na watoto wengi huko na mmoja, msichana ambaye ana miaka 16, Merhawit, alikuwa ametembea kilomita 300 na akiwa amembeba kaka yake mchanga mgongoni kutoka magharibi mwa nchi, wakati mapigano yaliposhika kasi… kilomita 300  ..!!! huku akiwa na malapa yaliyokatika. Hizo hadithi ni nyingi.  

QUOTE: Alikuwa nyota katika somo la fizikia, na sasa anatafuta chakula na hajaliona darasa kwa mwaka mmoja. -UNICEF James Elder 

Mbali na shida ya elimu, jimbo la Tigray pia liko kwenye dharura ya lishe, inayohusishwa na uporaji na uharibifu wa vituo vya matibabu na mifumo ya umwagiliaji ya gharama kubwa ambayo jamii za wakulima zinaitegemea. 

Elider ameongeza kuwa "Tumefanya tathmini hivi karibuni katika miji 13 na zaidi ya nusu ya miji hiyo visima havifanyi kazi. Ni muhimu kukumbuka kuwa hiii ilikuwa mifumo ya hali ya juu, iliyowasaidia mamia ya maelfu ya watu kwa kutumia jumeme wa jenereta lakini sasa yote imepora au kuharibiwa." 

Uharibifu na uporaji 

Vituo vya afya havijasalimika pia, na wahudumu wengi sasa hawafanyi kazi. 

Hii ni pamoja na kliniki mpya ya afya ya mama inayojishughulisha na upasuaji wa dharura kwa akina mama ambayo ilifunguliwa kilomita 100 kutoka mji wa Mekelle ambayo sasa imepora amesema Leader. 

"Kila kitu kimeporwa kuanzia mashine za X-ray, oksijeni, na magodoro ya kulalia wagonjwa vimekwenda. Daktari hapo aliniambia, kliniki ilikuwa na huduma zote za mama na mtoto kwa waliohitaji. Ilikuwa mahali pa kuokoa maisha. Hakukuwa na sababu ya vikosi kuja hapa. Walikuja hapa kwa uharibifu na uporaji.” 

Msemaji wa UNICEF pia amewasihi wale wote walio na ushawishi kwa watendaji wa jeshi wanaohusika katika mzozo kulaani ukiukwaji wa haki dhidi ya raia ikiwemo ukiukaji mkubwa na unaoendelea wa haki za watoto ambao umeripotiwa na waathiriwa. 

"Tuna wastani wa visa vitatu vya ukatili wa kijinsia vilivyoripotiwa, tukumbuke kwamba hii labda ni sehemu ndogo tu ya ukubwa wa tatizo kwa sababu kuripoti ni ngumu sana, kwa sababu za usalama na mambo ya kitamaduni ya aibu, na kadhalika. Nilisikia hadithi za kutia kiwewe za watoto walio na umri wa miaka 14, nikasikia ripoti za ubakaji unaofanywa na genge la watu. ” 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Flora Nducha
Audio Duration
3'6"
Photo Credit
© WFP/Leni Kinzli