Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bachelet: Uamuzi dhidi ya kesi ya Floyd ungalikuwa vinginevyo, ingalikuwa kituko dhidi ya haki

Bachelet: Uamuzi dhidi ya kesi ya Floyd ungalikuwa vinginevyo, ingalikuwa kituko dhidi ya haki

Pakua

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, amesema kitendo cha aliyekuwa polisi nchini Marekani kupatikana na hatia katika mauaji ya mmarekani mweusi Geroge Floyd  ni cha kihistoria na kwamba matokeo mengine ya kesi hiyo yangalikuwa kituko kwa haki.  Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Katika taarifa yake aliyotoa leo mjini Geneva, Uswisi, Bi. Bachelet amesema kitendo cha jana ushahidi wa ujasiri wa familia ya marehemu huyo na watu wengine waliotaka kuwepo kwa haki. 

Mshtakiwa katika kesi hiyo Derek Chauvin alipatikana na hatia katika makosa yote matatu kufuatia kuhusika kwake katika mauaji ya Floyd mwezi Mei mwaka jana. 

Bi. Bachelet amesema pamoja na uamuzi huo wa mahakama, bado kwa waathirika wengi wa asili ya Afrika na failia zao nchini Marekani na kwingineko, harakati dhidi ya haki zinaendelea, “mapambano ya kuona kesi za polisi kutumia nguvu kupita kiasi au kuua raia zinafikishwa mahakamani, achia suala la kuona zinapata ushindi, bado hayajakamilika.” 

Kamishna huyo amesema ukwepaji sheria wa vitendo vya uhalifu na ukiukaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na polisi lazima ukome na “tunahitaji kuona hatua thabiti za kuzuia mauaji holela yanayofanywa na polisi. Kama tulivyoshuhudia kwa uchungu katika siku na wiki za karibuni, marekebisho katika idara za polisi kote nchini Marekani bado hayatoshelezi katika kuzuia wamarekani weusi wasiuawe. Ni wakati wa kuondokana na maneno mengi kuhusu marekebisho na badala yake kufikiria kwa kina kile kinachofanywa na polisi nchini Marekani na kwingineko.” 

Bi. Bachelet amesema anatambua kuwa kuna hatua muhimu zinachukuliwa nchini Marekani, lakini juhudi hizo lazima zichagizwe, zipanuliwe na katu zisisahaulike pindi mtazamo wa umma unapoelekezwa kwenye masuala mengine. 

 

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Anold Kayanda
Audio Duration
1'44"
Photo Credit
Ann Sophie Persson