Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wajiandaa kufaidika na ujenzi wa bomba la mafuta la Africa Mashariki

Vijana wajiandaa kufaidika na ujenzi wa bomba la mafuta la Africa Mashariki

Pakua

Umoja wa Mataifa umekuwa ukisisitiza ushirikiano wa kimataifa katika kutatua changamoto za ulimwengu. Tanzania na Uganda ziko katika ushirikiano ambao unaelekea kutatua changamoto ya ajira na kukuza uchumi miongoni mwa wananchi wa ukanda huo wa Afrika Mashariki. Jumapili iliyopita, Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni na mwenzake wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan walikutana kwenye Ikulu ya Entebbe nchini Uganda na kutia saini mikataba muhimu inayoruhusu uzinduzi wa mradi wa pamoja wa ujenzi wa bomba la mafuta yasiyosafishwa la Africa Mashariki, EACOP na miradi mingine miwili ya kuuwezesha. Bomba hilo limeleta matunmaini sio tu kwa vijana bali pia kwa serikali zote mbili. Vijana wamekuwa wakichagizwa kusaka ujuzi wa kiufundi unaofaa ili waajirike na miradi ya mafuta inayotrajia kuleta ajira zaidi ya 160,000 nchini Uganda pekee.  Mwandishi wetu Uganda John Kibego ameandaa makala ifuatayo.

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Anold Kayanda
Audio Duration
3'53"
Photo Credit
World Bank/Arne Hoel