Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaamini maendeleo ya ulimwengu yanaweza kufanikishwa na kusimamiwa na vijana-Farida Makame 

Tunaamini maendeleo ya ulimwengu yanaweza kufanikishwa na kusimamiwa na vijana-Farida Makame 

Pakua

Ulimwengu ukiwa katika muongo wa kuelekea kufikia utimizaji wa malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 2030, shirika lisilo la kiserikali nchini Tanzania, Restless Development, lina imani kubwa kwa vijana kuwa wamekuwa na wanaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha malengo hayo hivyo uwekezaji mkubwa inabidi uendelee kuelekezwa kwa kundi hili hasa katika kuwajengea uwezo wa uongozi. Farida Makame ni meneja katika masuala ya ushirikianao na uwekezaji kwenye shirika hilo ambalo kwa zaidi ya miaka 25 limejikita katika kuangazia maendeleo ya vijana kwa kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi wa sasa na baadaye. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Farida Makame
Audio Duration
3'
Photo Credit
Restless Development Tanzania