Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo na vipaji vingine, mkombozi wa vijana, Kibera Kenya

Michezo na vipaji vingine, mkombozi wa vijana, Kibera Kenya

Pakua

Umoja wa Mataifa unaamini kuwa michezo inaweza kusaidia kuchukua jukumu katika kujenga mnepo na katika kupona dhidi ya janga la COVID-19. Vile vile Umoja wa mataifa unaamini kuwa michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo na amani. Nchini Kenya, katika mtaa wa mabanda, Kibera jijini Nairobi, wakfu wa UWEZA unajaribu kuwasaidia vijana kuweza kujitegemea kwa kutumia vipaji vyao. Miongoni mwa vipaji vinavyolengwa ni pamoja na uchezaji wa mpira wa miguu na uchoraji. Mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi amezungumza na Mkurugenzi wa Wakfu huu wa UWEZA, Jeff Okoth ambaye anaeleza kwa undani kuhusu shughuli za Wakfu huu. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Jason Nyakundi
Audio Duration
4'17"
Photo Credit
© Julius Mwelu/ UN-Habitat