Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wapongeza juhudi za UN kurejesha amani zapongezwa DRC

Wananchi wapongeza juhudi za UN kurejesha amani zapongezwa DRC

Pakua

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi hao Sheikh Abdul Kambale Bageni wa msikiti wa Mutwanga na Padri Ghislain Katsere wa Parokia ya Mutwanga  wanasema wanasema ulinzi wa amani kutoka Umoja wa Mataifa umesaidia sana kurejesha maisha katika hali yake ya kawaida na sasa watu wameanza kuishi bila hofu kama awali. Kwanza ni Sheikh Bageni, anasema, “tunasema asante sana kwa ujio wenu na tumesema asante kwa FRDC kwa kutulinda, na nyinyi pia kuongezeka ili amani iwe kubwa kabisa. Na kweli tangu mwezi Desemba watu walikimbia. Lakini walipoona FRDC na MONUSCO, tunaona kidogokidogo watu wanarudi.”

Naye Padri Katsere anasema, “namshukuru kwanza mwenyezi Mungu. Tulikuwa ndani ya shida ambayo inatutatiza. Ndugu zetu wamekufa wengi bila hesabu. Tuko ndani ya huzuni ambao ni Mungu na Mtume wake ndio wanajua. Ule umoja ambao MONUSCO na FRDC wanafanya tunauunga mkono na Mungu aiweke nguvu waweze kutusaidia na madhara ambayo tunakutana nayo.”

Nao akina mama kutoka Mji wa Mutwanga wameishukuru MONUSCO na Jeshi la Serikali kwa mchango mkubwa wanaoutoa katika kurejesha amani katika eneo lao ambapo sasa hivi wanaweza kufanya shughuli zao za maendeleo bila wasiwasi, kwanza ni Bi Marie Sambeti, “mimi ni Marie Sambreti nashukuru sana haya yote ambayo tunayaona ya urafiki katika ya jeshi la DRC yaani FRDC na MONUSCO, tunafurahi sana maana doria yao wanaifanya pamoja na ndio maana tunawashukuru sana.”
“Mimi ni Bi Saidat Said, tumeona kumbe ni watoto wa nyumbani wamekuja hapa. Hata kama nyinyi ni wageni lakini ni watoto wetu. Siku hizo bora tunalala nyumbani. Tukiwaona tunapata imani kuwa tunalindwa.” 

Naye Bi Saidath Said anaongeza,  “mimi ni Bi Saidat Said, tumeona kumbe ni watoto wa nyumbani wamekuja hapa. Hata kama nyinyi ni wageni lakini ni watoto wetu. Siku hizo bora tunalala nyumbani. Tukiwaona tunapata imani kuwa tunalindwa.” 

Kwa muda mrefu Mji wa Mutwanga ulikuwa umekimbiwa na wakaazi wake kufuatia mauaji yaliyokuwa yakiendeshwa na vikundi vya kihalifu lakini kutokana juhudi zinazofanywa na Jeshi la Serikali ya DRC kwa kushirikiana na MONUSCO kurejesha amani, wakazi wake wamekuwa wakirejea siku hadi siku. 

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Tumaini Bigambo
Audio Duration
2'35"
Photo Credit
MONUSCO/Michael Ali