Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Uganda wataka haki ya ardhi kwa kurekebisha sheria ya ndoa na talaka.

Wanawake Uganda wataka haki ya ardhi kwa kurekebisha sheria ya ndoa na talaka.

Pakua

Lengo namba 5 la Malengo ya Umoja w mataifa ya maendeleo endelevu linaangazia usawa wa kijinsia likilenga kufanya mageuzi ili kuwapa wanawake haki sawa kwa rasilimali za kiuchumi, na pia kupata umiliki na udhibiti wa ardhi na aina nyingine za mali, huduma za kifedha, urithi na maliasili, kwa mujibu wa sheria za kitaifa. 

Mojawapo ya viashiria vya kufanikiwa kwa lengo hilo ni pale ambapo kutakuwa na uwiano wa nchi ambazo mfumo wa kisheria (pamoja na sheria ya kimila) unahakikishia haki sawa za wanawake kwa umiliki wa ardhi na au udhibiti. 

Kwa msingi huo, wanawake nchini Uganda wanaendelea na harakati za kujaribu kurekebisha sheria ya ndoa ambayo bado haimtambui mwanamke katika haki ya kurithi mali zilizoko kati yake na mumewe ikiwemo ardhi isipokuwa tu pale anapokuwa ameolewa rasmi kimila, kusajili ndoa serikalini au kanisani jambo ambalo linaweza kukwamisha usawa wa kijinsia. Sheria hii inatekelezwa licha ya takwimu kukadiria wanawake zaidi ya asilimia sitini kuwa wanaishi katika ndoa zisizo rasmi, hali inayowatumbukiza wanawake katika madhila makubwa hasa baada ya kupoteza waume wao. 

Mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego ameangazia suala hilo na kutuandalia makala ifuatayo.  

 

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
Pete Muller for the ICC