Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana waunda roboti ya kusaidia watu wenye ulemavu

Vijana waunda roboti ya kusaidia watu wenye ulemavu

Pakua

Hawana kisomo cha chuo kuu lakini ujuzi wao katika masuala ya teknolojia ya kuunda roboti inayoweza kusoma na kuelewa anachofikria mwanadamu na ni uvumbuzi ambao umewashangaza wengi. Moses Njoroge na David Gathu ni wavumbuzi walio na karakana yao ndogo eneo la Kikuyu kaunti ya Kiambu nje kidogo ya mji wa Nairobi nchini Kenya, ambapo kwa kipindi cha miaka 10 wamejikita katika kuunda roboti inayoweza kuwasaidia watu walio na ulemavu wa miguu na mikono kujihudumia. Mwandishi wetu nchini Kenya Jason Nyakundi amezungumza nao akianza na Moses.
 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Jason Nyakundi
Audio Duration
4'35"
Photo Credit
UN/ Jason Nyakundi