Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutumie misimu ya matunda kila wakati ili kupata virutubisho kwa bei nafuu

Tutumie misimu ya matunda kila wakati ili kupata virutubisho kwa bei nafuu

Pakua

Tukiwa bado katika mwaka wa mbogamboga na matunda, mtaalamu wa lishe ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la lishe la Nutrition International Kenya, Bi. Martha Nyagaya anashauri watu wawe wanatumia misimu ya matunda kuhakikisha wanakula matunda ya misimu hiyo ili kuepuka gharama na kuepuka kula tunda moja tu kwa kipindi chote kwani matunda na mbogamboga tofautitofauti zina manufaa tofautitofauti mwilini. Kupitia mahojiano haya yaliyofanywa na mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi, Bi. Nyagaya anaanza kwa kueleza umuhimu wa kuhakikisha kila mlo unakuwa na mchanganyiko maalum wa vyakula.

Audio Credit
Anold Kayanda/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'27"
Photo Credit
© FAO-Magnum Photos/Alex Webb