Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wa kike wahimizwa kupigania haki za kumiliki ardhi Uganda.

Vijana wa kike wahimizwa kupigania haki za kumiliki ardhi Uganda.

Pakua

Wiki hii dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo sehemu mbalimbali wanawake waliitumia kuonesha kero zao na kutiana moyo. Nchini Uganda, wanawake katika wilaya ya Buliisa wameandamana hadi Makao Makuu ya wilaya hiyo kuwasilisha malalamiko yao wakiitaka serikali ishughulikie changamoto yao ya kunyimwa haki ya kumiliki ardhi.

Shirika la kiraia la NAPE limesajili wanawake takribani 100 wakisaka huduma za sheria baada ya kujikuta katika hatari ya kunyanganywa ardhi zao au kutofidiwa na kufurushwa majumbani baada ya kupoteza waume zao kuanzia Machi mwaka jana na Januari mwaka huu katika eno la Ziwa Albert pekee. Vijana wa kike wamehimizwa kuwa mstari wa mbele kupigania haki zao kama anavyosimulia John Kibego katika makala ifuatayo.

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kibego
Audio Duration
3'51"
Photo Credit
UN/ John Kibego