Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi yameacha kovu kwa wenyeji wa Ziwa Albert, Uganda.

Mabadiliko ya tabianchi yameacha kovu kwa wenyeji wa Ziwa Albert, Uganda.

Pakua

Mafuriko makubwa ambayo yanayohusishwa na mabadiliko ya tabianchi, yameshuhudiwa katika meneo mengi duniani kote na yamekuwa yakiathiri watu kwa namna tofauti. Sudan, Sudan kusini, Uganda na India ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na hali hii hususani katika kipindi cha kuelekea mwishoni mwa mwaka jana wa 2020. Ili kufuatilia maisha ya walioathirika na hali hii, mwandishi wetu wa Uganda John Kibego, amezungumza na Nyanjura Nyangoma mwanamke anayelea familia ya watoto 14 pembezoni mwa Ziwa Albert. Mwanamke huyu ni sehemu ya watu zaidi ya laki moja walioathiriwa na mafuriko nchini Uganda, katikati ya janga la COVID-19. Je, hali ikoje hivi sasa? Ungana naye katika makala hii.

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kibego
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
UN/ John Kibego