Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

24 Februari 2021

24 Februari 2021

Pakua

Hii leo jaridani tunaanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako wananchi licha ya madhilla wanayopitia mashariki mwa nchi hiyo wanashikamana na wanasaidiana ili angalau kupunguza machungu. Kisha ni suala la mgao wa mlo shuleni ambao sasa umekwenda mrama kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19. Huko Amerika ya kati hali ya chakula nayo ni tabu. Makala leo tunamalizia mahojiano yetu na mtaalamu wa lishe huko Njombe mkoani Tanzania kuhusu umuhimu wa matunda mwilini tukizingatia mwaka wa kimataifa wa matunda na mboga mboga. Usisahau pia mashinani tunakwenda nchini Kenya kumulika jinsi watoto walivyorejea shuleni baada ya shule kufungwa kutokana na COVID-19. Mwenyeji wako leo ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
FLORA NDUCHA