Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 Februari 2021

23 Februari 2021

Pakua

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanzia na ripoti mpya ya shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO ikiangazia majukwaa mapya ya ajira duniani yakiwemo yale ya mtandaoni na faida na changamoto zake. Kisha anakwenda nchini DR Congo ambako kikongwe mmoja amekata tamaa ya maisha baada ya kufurushwa kwake mara tatu. Taarifa nyingine ni kutoka Lebanon ambako theluji pasi kifani yatishia maisha ya wakimbizi. Makala anabisha hodi mkoani njombe nchini Tanzania mtaalamu wa lishe anazungmzia faida za mboga na matunda. Mashinani anakwenda Zambia kuona jinsi mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari yamewawezesha kutambua masomo ya kuchukua ili kufanya ajira za ndoto zao. Karibu!

Audio Credit
FLORA NDUCHA