Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 Februari 2021

22 Februari 2021

Pakua

U hali gani siku ya leo Jumatatu Februari 22 mwaka 2021 na mwenyeji wako Flora Nducha anakueletea mada kwa kina akimulika lugha ya mama, kwa kuzingatia kuwa tarehe 21 mwezi Februari ni siku ya lugha ya mama duniani. Katika kutekeleza hilo Grace Kaneiya akiwa Nairobi, Kenya amefuatilia wito kwa watunga sera, waelimishaji na walimu, wazazi na familia kuimarisha dhamira zao katika kuhakikisha elimu kupitia lugha mbali mbali na ujumuishaji kati elimu ili kuibuka kutokana na athari za janga la virusi vya Corona au COVID-19. Hata hivyo tuna habari kwa ufupi miongoni ni kuuawa kwa Balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na watu wengine wawili wakati wa ziara ya programu ya mlo shuleni inayotekelezwa na shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP. Mashinani tunasalia huko DRC tukimulika mtafiti wa mti ulio hatarini kutoweka akiwa huko msitu wa hifadhi wa Yangambi.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'7"