Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 Februari 2021

19 Februari 2021

Pakua

Leo ni Ijumaa na kama ilivyo ada ni mada kwa kina na tunakwenda Darfur nchini Sudan hususan eneo la Khor Abeche ambako hatimaye wiki hii kambi ya Khor Abeche iliyokuwa inatumiwa na walinda amani wa Tanzania katika UNAMID imekabidhiwa rasmi kwa serikali ya Sudan kufuatia kukamilika kwa majukumu ya ulinzi wa aman jimboni humo. Koplo Japhet Chaula, afisa habari wa kikosi cha 13 cha Tanzania, TANZBATT-13 kwenye UNAMID ndiye alikuwa shuhuda wetu katika tukio hilo la wiki hii. Katika Habari kwa Ufupi tunamulika Ebola Guinea na DR Congo, Yemen hali si shwari milimani na pia madhila yanayokumba watoto wakimbizi wa ndani nchini DR Congo. Katika kujifunza Kiswahili tunakwenda Tanzania kupata maana ya neno UDINDO. Karibu na mwenyeji wako ni Grace Kaneiya akipeperusha jarida kutoka Nairobi nchini Kenya.

Audio Credit
GRACE KANEIYA
Audio Duration
12'41"