Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 Februari 2021

18 Februari 2021

Pakua

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanza na masuala ya mazingira ambapo ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema bado safari ni ndefu kukabili mabadiliko ya tabianchi. Kisha anabisha hodi Msumbiji ambako anaangazia msaada kwa manusura wa dhoruba kali Eloise. Baada ya hapo anakwenda baharí Hindi visiwani Comoro ambako mradi wa shirika la kazi duniani, ILO umeleta ajira za staha kwa wakazi maskini. Makala tunarejea tena Tanzania jijini Dar es salaam kumulika kilimo cha mboga mboga na matumizi ya muarobaini kukabili wadudu waharibifu. Mashinani anakwenda Somalia kuona mchango wa redio katika kuimarisha upatikanaji wa chakula, karibu!

 

Audio Credit
FLORA NDUCHA