Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 Februari 2021

16 Februari 2021

Pakua

Hii leo jaridani Flora Nducha aanza na ombi la dola milioni 222 kwa ajili ya wakimbizi wa Burundi waliosaka hifadhi nchi jirani za Tanzania, DRC na Rwanda. Kisha ni Burkina Faso ambako huko afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amefika na kujionea hali halisi ya madhila yanayokumba wakimbizi wa ndani waliofurushwa majimbo ya Kusini Magharibi na Kaskazini Magharibi kutokana na ghasia. Taarifa ya tatu tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Tanzania kikosi cha 7, TANZBATT_7 kimekabidhi majukumu kwa kikosi cha 8, TANZBATT_8 ili kuendelea kupeperusha bendera ya Umoja wa Mataifa katika muktadha wa ulinzi wa amani. Na mashinani tunakwenda nchini Kenya, makala tunabisha hodi Uganda kuangazia kilimo cha mboga za majani na matunda na manufaa yake. Karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'12"