Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 Februari 2021

11 Februari 2021

Pakua

Hii leo Jaridani Grace Kaneiya kutoka Nairobi Kenya anaanza Habari za UN akimmulika msichana kutoka Rwanda ambaye ni mhandisi wa magari kwenye kampuni ya magari ya Hyundai kwenye mji mkuu Kigali, ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi. Kisha anakwenda Cameroon ambako radio imekuwa mkombozi kwa watoto ambao hawajakwenda shuleni kwa miaka mitatu sasa kutokana na mzozo nchini mwao. Sudan Kusini nako ukosefu wa amani wasababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito kwa serikali kutekeleza haraka mkataba wa amani wa mwaka 2018. Makala anabisha hodi nchini Tanzania hususan mkoani Njombe kuona mtazamo wa wakulima wa mboga za majani na matunda katika kutambua mwaka huu wa mboga mboga na matunda na mashinani tunarejea katika sayansi ambako msichana kutoka Kenya anahamasisha watoto wa kike wasiogope masomo ya Sayansi, STEM. Karibu!

Audio Credit
GRACE KANEIYA
Audio Duration
13'38"