Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 Februari 2021

10 Februari 2021

Pakua

Jaridani hii leo Flora Nducha anaanza na taarifa ya changamoto kwa watengeneza chanjo dhidi ya COVID-19 duniani wakati huu ambapo chanjo za sasa zimeonekana kuwa dhaifu kwa mnyumbuliko mpya wa virusi vinavyosababisha Corona.  Anaangazia pia siku ya kimataifa ya mikunde hii leo ambapo taarifa inataja faida za mikunde kama vile maharagwe, kunde zenyewe, choroko na hata njugumawe. Nchini Uganda nako anabisha hodi kuona msaada wa UNICEF katika huduma za mama na mtoto na mashinani tunabisha hodi leo mashariki ya mbali, nchini Afghanistani. Makala tunakwenda Afrika hususa nchini Tanzania tukiendelea na mfululizo wa makala za mboga mboga na matunda na kusikia jinsi kilimo na biashara yake vinasaidia kaya kubadili maisha. Karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'4"