Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 Februari 2021

09 Februari 2021

Pakua

Jaridani hii leo Jumanne Februari 09 2021, Flora Nducha anaanzia Msumbiji kumulika msaada wa Umoja wa Mataifa kwa manusura wa kimbunga Eloise, wamejengewa makazi ya muda na huduma za kujisafi na maji safi. Kisha anakwenda Colombia ambako wakimbizi kutoka Venezuela wanazidi kumiminika wakikimbia madhila nchini mwao lakini taifa hilo mwenyeji linarasimisha uwepo wao. Taarifa nyingine ni kutoka Zimbabwe na shirika la FAO. Makala tunatamatisha awamu ya pili ya mahojiano kuhusu mboga na matunda huko Uganda na mashinani tunakwenda Somalia ambako msichana Soman kwa msaada wa mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na la mpango wa chakula duniani, WFP na wafadhili kutoka Ujerumani sasa anaweza kuhudhuria shule, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'29"