Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

05 Februari 2021

05 Februari 2021

Pakua

Leo Ijumaa ni mada kwa kina na Assumpta Massoi anakupeleka Nairobi Kenya ambako Grace Kaneiya katika kufuatilia utekelezaji wa mwaka wa kimataifa wa mboga mboga na matunda amevinjari kwa familia moja jijini Nairobi kuona mtazamo wao katika ulaji wa mboga za majani na matunda. Lakini kuna muhtasari wa habari ukiangazia sakata la Tigray nchini Ethiopia, hali ya kibinadamu Burkina Faso na wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuelekea siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake kesho jumamosi .Neno la wiki leo ni kujifunza methali, kitanda usichokilalia, hujui kunguni wake. Karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
10'39"