Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 Februari 2021

04 Februari 2021

Pakua

Hii leo jaridani Grace  Kaneiya kutoka Nairobi nchini Kenya anaanzia na taarifa kuhusu siku ya saratani duniani ikimulika changamoto za upimaji wa gonjwa hilo wakati huu wa janga la COVID-19. Kisha anakwenda Morogoro nchini Tanzania kumulika tatizo la lishe duni na makuzi ya mtoto, halafu anakupeleka Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako amani imerejea katika mji wa Bangassou uliokuwa kitovu cha mashambulizi tarehe 3 mwezi uliopita. Makala tunaendelea na mbogamboga na leo tunakwenda Uganda ambako mkimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC anaelezea vile ambavyo katika makuzi yao mboga za majani zilipatiwa umuhimu. Mashinani tunakutana na mtoto wa kike aliyekimbia kukeketwa. karibu!

Audio Credit
GRACE KANEIYA
Audio Duration
13'25"