Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 Februari 2021

03 Februari 2021

Pakua

Leo Jumatano Flora Nducha anaanzia huko Madagascar ambako ukame wa muda mrefu umesababisha njaa kali na watu kulazimika kutengeneza rojo la ukwaju na kunywa huku wakilumangia na udongo mweupe. Kisha anakwenda Tigray nchini Ethiopia ambako nako hali si hali kwa wakimbizi wa ndani wakimbiao mapigano na wale waliotoka Eritrea. Hata hivyo WFP ambalo ni shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa  limetangaza mpango wake wa kusambaza kwa haraka chakula kwa wenye uhitaji zaidi barani Afrika. Makala tunaendelea na mfululizo wa makala za mbogamboga na matunda na leo tunaelekea mkoani Njombe nchini Tanzania kwake Zawadi Kikoti. Mashinani tunammulika mkimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati ambaye amelazimika kukimbia nchi yake mara tatu. Karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
15'7"