Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 Februari 2021

02 Februari 2021

Pakua

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanza na ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu ikionesha kuwa wavulana wanaosafirishwa kiharamu idadi yao imeongezeka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Watu wengine wanasafirishwa pia kutumikishwa kwenye kuombaomba. Kisha atakufikisha Baidoa nchini Somalia kumulika hali ya kibinadamu na hatimaye Sudan Kusini ambako shule moja ya sekondari yaonesha uwezo wa wanafunzi wakimbizi. Makala tunabisha hodi mkoani Tabora nchini Tanzania kwa radio washirika Radio Uhai wakimulika umuhimu wa matunda kwa kuzingatia huu ni mwaka wa matunda na mboga mboga. Mashinani tunamulika harakati za UNICEF nchini Kenya kuhakikisha watoto wanakuwa salama shuleni wakati huu wa janga la COVID-19, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'59"