Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 Januari 2021

15 Januari 2021

Pakua

Leo Ijumaa ni mada kwa kina ambapo tunaangazia hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona au COVID-19 katika shule ya Joram G.M Academy iliyoko, Matasia kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Shule hiyo imefunguliwa tena baada ya kufungwa kwa muda mrefu kutokana na janga la COVID-19, hatua ambazo zilitangazwa na serikali. Tunamulika pia lugha ya kiswahili na leo kutoka Uganda kwake Aida Mutenyo, mwenyekiti wa Idara za Kiswahili katika Vyuo Vikuu Afrika Mashariki, tunaangazia maana ya sentensi. Usisahau Habari kwa Ufupi ikiangazia habari muhimu kwa siku  ya leo. Mwenyeji wako jaridani ni Flora Nducha huku Grace Kaneiya akikufikisha Kajiado nchini Kenya, karibu!

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'48"